Watu watatu wamefikishwa mahakama ya
wilaya ya Chato kusomewa shitaka la mauaji ya mtoto Yohana Bahati
aliyeibiwa hatimaye kuuwawa tarehe 15 Februali katika kitongoji cha
mapinduzi wilayani Chato mkoani Geita.
Akizungumza na waandishi wa habari,
kamanda wa polisi mkoa wa Geita Sacp Joseph Konyo amesema watu wengine
wawili bado wanahojiwa na jeshi la polisi ili kupata ushahidi
unaojitosheleza katika kesi hiyo, amewataja watu waliofikishwa
mahakamani ni Bahati Misalaba ambaye ni baba wa Yohana, Juma Lupembe
Kilebelo, Manyanda Mandege almaarufu Makongoro mkazi wa wilaya ya Mbogwe
na mchimbaji wa dhahabu.
Kamanda konyo amesema jeshi la polisi
linaendelea na juhudi za kuwakamata wauwaji wa kukodiwa wanaofanya
mauaji hayo kwa ujira mdogo wa laki moja ili kudhibiti vitendo vya
mauaji katika maeneo ya kanda ya ziwa.
Katika tukio jingine jeshi la polisi
limefanikiwa kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu watatu
wanaosadikika kuwa ni majambazi wazoefu wa kuteka magari barabarani na
kuvamia maduka ya fedha mkoani Geita, watu hao Niosca John Bosco, Kapuru
Msigwa ustaadhi, na Elias Shigilimelo Bambala.
via>>ITV
via>>ITV
0 Comments