Baada ya ile story iliyozagaa mitandaoni kuwa mwanadada Amanda poshy
anatumia ARV (Dawa ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI) hatimaye
leo, mwanadada huyo ameamua kuudhihirishia umma kuwa yeye yuko safi, na
habari hizo ni uzushi tu na yenye lengo la kumchafua kwenye jamii baada
ya kuamua kupima na kuweka majibu yake ya vipimo vya “ngoma” hadharani
kwenye mtandao mmoja wa kijamii.
Katika picha hiyo mwanadada huyo aliandika kuwa ni vizuri kucheki afya
yako mara kwa mara, picha iliyokuwa ikionesha kuwa majibu hayo ya ngoma
yanaonesha kuwa mwandada huyo yuko HIV NEGATIVE.
Je wewe umepima? Majibu yanasemaje? Au ulikimbia majibu?
0 Comments