Biionea Alhaji Aliko
Dangote amekabidhiwa hekari 2,500, katika halmashauri ya Wilaya ya
Mtwara ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji kutoka
kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mfanyabiashara maarufu
Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya
Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono
kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata
ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari
yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye
kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa na
wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika
na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine
ya maendeleo
Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa
0 Comments