Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
Watu
hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi
wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
Kufuatia
shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red
Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.
Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kimeanzishwa chini ya mti.
Mwanafunzi
wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati
wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua
milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamuama wakristo.
''Kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.Kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',ameliambia shirika la habari la AP.
Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.
Mwandishi
wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu
cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:
Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''Ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka upande wa pili.@ntvkenya".
0 Comments