Siku
moja baada ya kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima kuachiwa kwa
dhamana na jeshi la polisi, maaskofu na wachungaji kutoka makanisa
mbalimbali wameibuka na kuwataka wakristo kote nchini kuwa katika hali
ya utulivu wakati sakata la askofu Josephat Gwajima likishughulikiwa na
vyombo vya sheria.
Wakizungumza
jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, maaskofu na wachungaji
kutoka makanisa mbalimbali, licha ya kukataa kusema walichozungumza na
mkuu wa jeshi la polisi nchini, wamewataka wakristo kote nchini kuwa
katika hali ya utulivu huku wakiendelea kuenzi tunu ya amani iliyopo
hapa nchini wakati vyombo vya sheria vikiendelea kushughulikia sakata
hili la askofu Josephat Gwajima.
Wakizungumzia
kauli ya askofu Gwajima aliyotamka kwa vyombo vya habari wakati akitoka
kuhojiwa katika kituo cha polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam
kuhusu kusimamia kauli zake, maaskofu hao wamesema kwamba askofu Gwajima
hawawezi kusaliti kauli iliyotolewa na jukwaa la waakristo Tanzania na
akifanya hivyo hata wao watamshangaa na ndio maana askofu Gwajima
aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye kama mtumishi wa mungu lazima
akemee jambo analoona haliendi sawa.
Maaskofu
hao na wachungaji wamempongeza kwa dhati askofu mkuu wa jimbo kuu la
Dar es Salaam Cadinali Polcarp Pengo kwa kutangaza kusamehe yote
yaliyotokea kati yake na askofu Josephat Gwajima kwani kwa kufanya hivyo
ndio ukiristo wa kweli.
0 Comments