Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Arusha zimesababisha madhara
makubwa baada ya kubomoa mabwawa 8 yanayotegemewa kwa maji ya matumizi
ya binadamu na wanyama kuharibu zaidi ya hekari arobaini za mazao ya
mahindi pamoja na kubomoa madaraja katika kijiji cha Esilalei wilaya ya Monduli na kuathiri zaidi ya watu elfu nne.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika kijiji cha Esilalei na kushuhudia uharibifu
mkubwa katika mashamba mabwawa na madaraja ambayo yamesababisha kufunga
mawasiliano kati ya kata ya Esilalei na maeneo mengine huku wakazi wake
wakieleza walivyo athirika na tukio ilo lilitokea kwa mara ya pili
katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.
Mwenyekiti wa kijiji cha Esilalei Lemweli Sembweye amesema athari
hizo pia zimesababisha kufungwa kwa shule ya msingi kijijini hapo
kwa kuwa hata miundo mbinu ya shule pamoja na sehemu zingine za huduma za
jamii pia vimeathirika.
Akielezea
hasara iliyotokea diwani wa kata ya Esilalei Madunga Nangali amesema
hadi sasa hakuna huduma ya maji katika eneo ilo kwani
zaidi ya mabwawa yaliyobomoka hakuna chanzo kingine cha maji na wana
mashaka kuwa idadi kubwa ya wakazi wake watakuwa wameathirika kiafya
kutokana na hali hiyo.
Via>>ITV
0 Comments