Kuna
ule usemi usemao elimu haina mwisho
au kawia Ufike!! Ni vigumu kuamini eti bibi kama huyu anaweza kuwa na
moyo wa kuendelea kusoma kwa miaka aliyonayo kwa sasa, Marie Hunt
kuingia kwenye headlines kwa kuhitimu masomo ya kidato cha sita akiwa na
umri wa miaka 103.
Marie angeweza kuhitimu elimu hiyo miaka 87 iliyopita lakini haikuwa hivyo kutokana na sababu mbalimbali zilizomkabili.
Marie
anayeishi katika mji wa Wisconsin, Marekani alishindwa kuendelea na
masomo yake kutokana na kukosa fedha na hivyo kubaki nyumbani
kuwaangalia wadogo zake.
Hunt alitakiwa kumaliza masomo yake
mwaka 1928 lakini siku moja alitamani kutimiza ndoto zake za kusoma na
sasa amemaliza masomo ya Diploma katika shule River Valley High School.
Hata hivyo hakueleza nia ya kuendelea na masomo zaidi ya hapo lakini amesema angeweza kuwa mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu.
0 Comments