KUFUATIA kauli ya Wema
Sepetu ya hivi karibuni kuwa hawezi kupata mtoto wa kumzaa, mastaa wa
fani mbalimbali wamejitokeza kumtuliza moyo, wakiongozwa na hasimu wake
wa karibu, Kajala Masanja, ambaye amesema hana sababu ya kukata tamaa,
kwani bado ni mdogo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
Akizungumza na gazeti
hili baada ya kuombwa maoni yake, Kajala alielezea masikitiko yake juu
ya hali ya rafiki yake wa zamani, lakini akasema anaamini hana tatizo
kubwa la kumfanya asipate kabisa mtoto, isipokuwa anadhani bado
hayampata mtaalamu sahihi wa masuala ya wanawake anayeweza kumsaidia
tatizo alilonalo.
“Namuombea sana kwa
Mungu, lakini sitaki kabisa kuamini kama hawezi kupata mtoto katika
maisha yake, mbona bado kijana sana, atapata tu bwana,” alisema Kajala,
ambaye ana mtoto aitwaye Paula.“Sitaki kuamini, roho inaniuma sana,
namshauri Wema asiumie wala kuwa mnyonge.
Na watu waache kumuumiza
kwa maneno ya kebehi, lakini kama Wema akiwa tayari kulea mtoto wa
mwenzake, anione, nina imani atapata mtoto atamlea na kumtunza kama
wake.
Wastara Juma.
“Naomba achukue mfano
wangu mimi Wastara, Mungu kanipokonya mguu kanipa watoto, natumia mguu
wa bandia na ninatembea lakini Wema amepewa kila kitu kasoro mtoto,
atumie mtoto ambaye siyo wa kumzaa amlee kama wa kwake na hapo machungu,
huzuni na mawazo vitaisha na atamzoa kama wa kwake,” alisema Wastara
Juma.
Wengine waliompa pole na
kumtakia nguvu kukabiliana na tatizo lake ni pamoja na Jini Kabula,
Salome Urassa ‘Thea’, Aisha Bui, Amanda Posh na Baby Madaha ambaye
alisema;
Aisha Bui.
“Mtoto siyo mwisho wa
maisha, kuna mastaa wengi tu ambao hawana watoto na wanaishi kwa amani
kama Oprah, Tyra Banks na wengineo, hivyo siyo ishu kubwa kihivyo, watu
waache kumsakama Wema, mimi mwenyewe sina mpango wa kuwa na mtoto.”
0 Comments