Mwanamke mmoja, mkazi wa
Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, anadaiwa kuanzisha danguro la
wasichana na kuendesha biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia moja.
Mwanamke huyo
anayefahamika kwa jina la mama Uzuri, anadaiwa kuwachukua wasichana hao
kutoka vijijini kwa kuwadanganya kuwa anakwenda kuwatafutia kazi mjini.
Inadaiwa kuwa fedha anazopata kutokana na biashara hiyo, huzitumia kama gharama ya kuwatunza wasichana hao.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti, wasichana hao (majina yanahifadhiwa), walidai kuwa mwanamke
huyo aliwachukua vijijini kwao kwa ahadi ya ajira za ndani.
Wakielezea undani wa
biashara hiyo, walisema wanaume wengi wamekuwa wakiwalazimisha kufanya
mapenzi bila kinga (kondom), kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo
kunawanyima starehe ya tendo hilo.
Suzana (sio jina lake
halisi), alisema makazi yao ni nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo
hulelewa katika mazingira mazuri, na kati yao kuna makahaba na wasagaji.
Alisema, mwanzo walipoanza biashara hiyo walipata wakati mgumu lakini kadiri siku zinavyokwenda waliizoea.
Alisema baadhi yao
wanachukuliwa na wanaume zaidi ya mmoja kwa siku na wakati mwingine
hugeuka kuwa walimu kwa wasichana wapya wanaoletwa kutoka vijijini.
“Wakati nachukuliwa kwa
wazazi wangu, mwajiri wangu aliwaeleza kwamba nakuja kufanya kazi za
ndani kwa ndugu yake, na kamwe sitopata madhara yoyote kutokana na
ulinzi na usimamizi nitakaoandaliwa, lakini baada ya kufika hali ikawa
tofauti," alisema na kuongeza:
“Nilipokelewa vizuri na
wasichana wenzangu niliowakuta, lakini nilishangazwa na kauli ya mwajiri
wangu kuwa nahitaji kufanyiwa ukarabati wa kutosha, na akatoa agizo
kutofanyishwa kazi yoyote badala yake nipumzike na nitaandaliwa kila
kitu ninachokitaka, lakini atakaponituma sehemu na wenzangu nikatekeleze
kama atakavyoniagiza, alisema Suzana.
Uchunguzi wa NIPASHE
katika mahojiano na mwanamke huyo, alisema ni vigumu kuiacha biashara
hiyo kwa sababu aliianzisha siku nyingi akiwa na wasichana watano.
Alisema wasichana hao
amewaajiri kwa gharama kutokana na shughuli wanazozifanya, na
wanapokwenda kijijini kwa wazazi wao, huwagharamia matumizi na zawadi
kwa familia zao.
Alisema gharama za
biashara hiyo hutofautiana kulingana na kiwango cha mteja, lakini kwa
wale wanaofanyiwa tendo hilo kinyume na maumbile, wateja hutozwa Sh.
20,000, na ngono ya kawaida Sh. 5,000 hadi Sh.10,000 kwa mara moja.
Aidha, alisema wanaofanya tendo hilo kwa jinsia moja (wasagaji), gharama zake hazitofautiani.
“Kifupi wasichana wangu
wanajituma hata wateja wenyewe wanawakubali ndani na nje ya Dar es
Salaam, lakini biashara ina msimu, kuna wakati inakulipa na wakati
mwingine inasuasua.
“Kikubwa ni ujanja na
namna ya kuwaandaa wasichana, kwa bahati nzuri katika familia zao hakuna
anayejua kazi anayoifanya mtoto wake zaidi ya ‘house girl’. Ni marufuku
kutoa siri ya kazi hivyo ni lazima niwekeze kwao kwa gharama yoyote
maana najua wanachokifanya mjini,” alijitapa mwanamke huyo.
Alisema ingawa anajua
kuna maradhi lakini amekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwao ili waweze
kujikinga na magonjwa hatari yanayoenezwa kwa njia ya ngono pamoja na
ugonjwa hatari wa Ukimwi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments