Shirika la Afya Duniani, WHO,
linasema inavyoelekea dawa ya kuua magugu ndyio chanzo cha vifo vya watu
18 vilivyotokea kusini-magharibi mwa Nigeria, bila ya sababu kujulikana.
Katika
siku chache zilizopita wakazi katika jimbo la Ondo wamekufa saa chache
baada ya kuhisi macho hayaoni sawa sawa na kuumwa na vichwa baadaye wanazimia.
Msemaji wa WHO ameeleza kuwa ukaguzi uliofanywa hadi sasa kutafuta virusi au bacteria haukugundua kitu.
Amesema kwa sasa mawazo yao ni kuwa vifo hivyo vilisababishwa na dawa ya kuua magugu.
Via>>BBC
0 Comments