Kivutio kingine kikubwa kwenye hili shindano lililoandaliwa na kituo kikubwa cha TV cha Ufaransa, TRACE Urban, kilikua ni Akon, mwimbaji maarufu aliyezaliwa St. Louis, Missouri Marekani miaka 41 iliyopita lakini maisha yake ya utoto yakapitia pia mikononi mwa Senegal.
Kwenye
picha ya kwanza juu ni Akon akiwa Jaji pamoja na Lynnsha na Devyne
Stephens ambao wakati Mayunga anaimba wimbo wa mwisho kabla ya mshindi
kutangazwa, walisimama kwa ishara kwamba wamemnyooshea mikono Mtanzania
huyu kwa ukali au kipaji kikubwa alichokionyesha kwenye uimbaji.
Super star huyu mpya amezaliwa ambapo miongoni mwa vitu atakavyovifanya ni kuungana na Akon kwenye studio yake huko Marekani kwa ajili ya kurekodi single yake ya kwanza (Mayunga)
0 Comments