Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza anayedaiwa kupiga mimba mbili nje ya ndoa na kutelekeza watoto.
Aibu!
Peace Sylvester (36), mkazi wa Kijenge Juu jijini amefungua madai
mazito kwenye Kituo Kikuu cha Polisi, Arusha kwa majadala mawili,
AR/RB/4404/2015 KUTISHIA KUUA KWA MANENO na AR/RB/5290/2015 KUTELEKEZA
FAMILIA dhidi ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) Dayosisi ya Karagwe, Kagera, Benson Bagonza.
Peace alidai Askofu
Bagonza ni mzazi mwenzake kwa kuzaa naye watoto wawili, Piana Bagonza
(6) na Bariki Bagonza (3) lakini akadai amemtelekeza hivyo kuwa na
maisha magumu katika kuwalea watoto hao.
AANIKA HISTORIA NDEFU
Peace alisema alianza
kufahamiana na askofu huyo mwaka 2006 mjini Karagwe, Kagera akiwa ni
muumini wa kanisa hilo akimtumikia Mungu kwa kuimba kwaya ya kanisa.
Alisema katika kuonana mara kwa mara na askofu huyo ndipo uhusiano ukaanza
lakini kwa makubaliano ya kutunza siri.
“Askofu aliniambia ana
mke lakini ananipenda na anataka kuwa na uhusiano na mimi. Aliniahidi
kunisaidia masuala mbalimbali iwapo nitamkubalia.
“Baada ya muda niliamua
kumkubalia, tukawa na uhusiano na tulikuwa tunakutana mara kwa mara.
Ilipofika mwaka 2008 nikapata ujauzito wa mtoto wa kwanza,” alisema
Peace.
AHAMIA ILEMELA, MWANZA
Mwanamke huyo aliendelea
kudai kuwa, baada ya kupata ujauzito, askofu huyo aliamua kumhamishia
Ilemela mkoani Mwanza na kumpangishia chumba ambapo mwaka 2009
alijifungua mtoto wa kike, Piana.
AHAMIA ARUSHA
Peace aliendelea kudai:
“Mtoto wangu alipofikisha umri wa miaka miwili, yaani mwaka 2010, askofu
alinihamishia hapa Arusha na kunipangia chumba eneo la Kijenge Juu na
kunitafutia kazi kwenye Hoteli ya Safari (New Safari Hotel). Hii hoteli
inamilikiwa na KKKT.”
Watoto anaodaiwa kuwatelekeza |
Alisema:
“Askofu alikuwa akija hapa Kijenge kumsalimia mtoto na kumwachia
matumizi mbalimbali huku akisisitiza kutunza siri zaidi.”
ANASA MIMBA YA PILI
“Ilipofika mwaka 2011
nilipata ujauzito mwingine wa askofu ila cha kushangaza nilipomfahamisha
aliniambia hataki kusikia taarifa hizo.
“Niliweka msimamo wa kutotoa ujauzito na yeye akasitisha huduma mbalimbali ikiwemo fedha za malipo ya chumba alichonipangia.
“Alianza kunipigia simu
na kunitisha kuniachisha kazi aliyonitafutia hotelini bila kupewa malipo
yoyote. Alikuwa akinitumia watu mbalimbali kunitishia maisha.
“Kutoka na hali hiyo
nililazimika kumtafuta kiongozi mmoja wa ngazi ya juu kanisani na
kumwambia jinsi askofu alivyonitelekeza kwa zaidi ya miaka minne bila
kunihudumia nikiwa na watoto wake wawili.
“Hata hivyo, kiongozi
huyo aliniambia atalishughulikia suala langu, lakini hadi sasa hakuna
kinachoendelea na nikimkumbusha amekuwa akinijibu kwa ukali na kunikatia
simu.”
WATOTO HAWAENDI SHULE
Peace alisema: “Kwa sasa naishi kwa shida na watoto. Hawaendi shule baada ya kukosa ada.”
ASKOFU ANASEMAJE?
Akizungumza kwa simu na
mwandishi wa habari hizi huku akihifadhiwa sauti, Askofu Bagonza alikiri
kumtambua Peace kama mzazi mwenzake ila alisema si kweli kama hamtumii
matumizi.
“Mbona fedha huwa
namtumia labda ameamua kunichafua tu. Hata juzi nimemtumia shilingi
250,000 iweje asema simhudumii?” alisema askofu huyo na kukata simu.
Kwa upande wake, Peace
alipoulizwa kuhusu kutumiwa kiasi hicho cha fedha, alisema: “Fedha hizo
nilizipokea kutoka kwa wakala wa M-Pesa baada ya jambo hilo kulifikisha
kwenye vyombo vya dola (polisi).
”Taarifa zilizolifikia zinaeleza kuwa mwanamke huyo ameitwa Karagwe kwenda kuongelea suala hilo.
Chanzo: GPL
0 Comments