Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kuandikisha wapigakura kwenye mikoa ambayo ni ngome ya CCM na kwamba ile yenye upinzani itaandikishwa kwa kulipua ili watu wengi wenye sifa ya kupiga kura wasiandikishwe.
NEC
ilianza kuboresha Daftari la Wapigakura kwa kuandikisha wananchi wa
Mkoa wa Njombe, ambako watu 300,080 waliandikishwa kati ya 392,634
waliotarajiwa na sasa inaelekea mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Iringa
baada ya kupokea mashine nyingine 1,600. Kazi hiyo itaendelea kwenye
mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma wakati mashine 1,600 zaidi
zitakapowasili.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva amesema hilo ni jambo
jipya kwake kwa kuwa hawakuangalia suala hilo wakati wa kupanga mikoa
hiyo.
Akizungumza
jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada
ya kuwasili nchini akitokea Marekani, Dk Slaa alisema wamegundua kwamba
mwishoni mwa kazi ya uandikishaji kwenye mikoa ambayo ni ngome ya vyama
vya upinzani, watu wengi hawataandikishwa.
“Tumegundua
hujuma zao, NEC wameanza kuandikisha wapigakura kwenye mikoa ambayo ni
ngome ya CCM. Huko wanajitahidi kuandikisha wapigakura wote na
wanachukua muda mrefu,” alisema Dk Slaa akionekana kurejea Mkoa wa Njombe ambako NEC imetumia takriban miezi miwili kuandikisha wapigakura.
“Mikoa
yenye ngome ya Chadema na vyama vingine vya upinzani itakuwa ya mwisho
kuandikisha wapigakura na uandikishaji huo utakuwa wa harakaharaka ambao
utawaacha mamia ya watu bila kuandikishwa kwa sababu muda utakuwa
hautoshi,” alisema Dk Slaa.
Alisema suala hilo linaweza kuvuruga uchaguzi, hasa ikizingatiwa kwamba mchakato wa uandikishaji umekuwa na sintofahamu nyingi.
Kwa
mujibu wa matokeo ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, CCM ilivuna
kura 128,809 katika majimbo matatu ya mkoani Njombe (Njombe, Ludewa na
Makete) wakati huo ukiwa ndani ya Mkoa wa Iringa. Chadema ilifuatia kwa
kupata kura 36,928 na CUF/NCCR zilipata kura 1,670
Kwa
kujumuisha kura hizo na majimbo mengine ya Iringa CCM ilipata jumla ya
kura 299,799 ikifuatiwa na Chadema iliyopata kura 76,010. CUF na
NCCR-Mageuzi zilipata jumla ya kura 3,137. Hadi sasa upinzani una mbunge
mmoja tu kwenye mikoa hiyo miwili, Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa
Mjini.
Kwenye
uchaguzi wa Rais mwaka 2010 mkoani Lindi, mgombea wa CCM alipata kura
150,118 akiwa mbele ya mgombea wa CUF aliyepata kura 64,875 wakati
wagombea wa Chadema na NCCR walipata jumla ya kura 12,880.
Wapinzani wana wabunge wawili mkoani Lindi ambao ni Selemani Bungera wa Kilwa Kusini na Salum Barwany wa Lindi Mjini, wote kutoka CUF.
Wapinzani wana wabunge wawili mkoani Lindi ambao ni Selemani Bungera wa Kilwa Kusini na Salum Barwany wa Lindi Mjini, wote kutoka CUF.
Mkoani
Mtwara, mgombea urais wa CCM alipata kura 213,844 akimuacha mbali
mgombea wa CUF aliyepata kura 81,953, huku wagombea wa Chadema na NCCR
wakipata jumla ya kura 82,233. Hakuna mbunge kutoka upinzani mkoani
Mtwara.
Takwimu
za 2010 pia zinaonyesha kuwa mkoani Ruvuma, mgombea urais wa CCM
alipata kura 198,090, akimuacha kwa mbali mgombea wa Chadema aliyepata
kura 36,044, CUF (28,873) na NCCR kura 397.
“Tunamwomba
Rais Jakaya Kikwete atuepushe na vurugu zinazoweza kutokea. Kwa kuwa
anamaliza muda wake Oktoba 28, mwaka huu, ahakikishe kwamba NEC
inaandikisha watu wote bila kupendelea mikoa yenye ngome ya CCM,” alisema.
Alisema
Rais anatakiwa ahakikishe kwamba kwa kutumia bajeti ya mwaka wa fedha
wa 2015/16, NEC inawezeshwa kupata fedha za kutosha ili iweze
kuandikisha watu kwa ufanisi zaidi.
“Tungependa
Rais Kikwete aiache nchi ikiwa salama kwa sababu kasoro zilizojitokeza
katika zoezi hili ni nyingi na zikiendelea zinaweza kuvuruga uchaguzi...
uchaguzi ndiyo kipaumbele chetu mwaka huu, ”alisema.
Alisema
Serikali ihakikishe inashinikiza kuingizwa kwa vifaa vya BVR ambavyo
vinaingia kwa mafungu ili wananchi wenye sifa waweze kuandikishwa.
Hadi
sasa kati ya mashine za BVR 8,000 ambazo zinatakiwa kuingizwa nchini
kwa ajili ya kazi hiyo, ni 2,098 tu ndizo ambazo zimeshawasili.
NEC yajibu
Akijibu madai hayo Jaji Lubuva alisema hilo ni jambo jipya kwake:“Hatufahamu kwamba mikoa hiyo ni ngome ya CCM,” alijitetea Jaji Lubuva.
“Tumeanza kuandikisha bila kujali kwamba hiyo ni ngome ya chama fulani cha siasa.” Alisema Dk Slaa anachotakiwa kufahamu ni kwamba kila mwananchi mwenye sifa atakayejitokeza kuandikishwa, ataandikishwa.
“Tumeanza kuandikisha bila kujali kwamba hiyo ni ngome ya chama fulani cha siasa.” Alisema Dk Slaa anachotakiwa kufahamu ni kwamba kila mwananchi mwenye sifa atakayejitokeza kuandikishwa, ataandikishwa.
“Sisi hatuangalii ngome za vyama vya siasa, kazi yetu ni kuandikisha bila kujali hapa ni ngome ya nani,” alisema.
Ziara ya Marekani
Dk
Slaa, ambaye aliambatana na mkewe, Josephine Mushumbushi alisema
wamekubaliana kuanzisha ushirikiano hasa katika nyanja za kiuchumi na
Jimbo la Indiana.
“Tumekubaliana
kwamba tukiingia Ikulu tutapenda kuwa na wawekezaji, lakini tofauti na
ilivyo sasa. Watakaotaka kuja kuwekeza nchini watatakiwa kufanya hivyo
kwa kufuata masharti yetu na siyo masharti yao,” alisema.
Dk
Slaa aliwasili jana saa 2.30 asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar
Airways na kulakiwa na wafuasi wa chama hicho waliokuwa na bango
linalosomeka, “Karibu nyumbani rais wa awamu ya tano Dk Willibrod Slaa.”
Dk
Slaa alikwenda Marekani kwa mwaliko wa Gavana wa Jimbo la Indiana, Mike
Pence pamoja na taasisi mbalimbali, vikiwamo vyuo vikuu, baada ya
kutambua mchango wake na wa chama chake katika masuala ya kisiasa na
kijamii katika maendeleo ya Bara la Afrika.
Akifafanua,
alisema alipata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za vyuo na
kujionea namna nchi hiyo inavyothamini tafiti za wasomi.“Wenzetu
wamewekeza kwenye tafiti, moja ya vipaumbele vikubwa kwa Serikali yao ni
kutoa fedha za kutosha kwenye tafiti tofauti na hapa nchini ambako
utafiti siyo kipaumbele chetu,” alisema.
Alisema
pia alitembelea shamba la mifugo lenye ng’ombe wa maziwa 15,000 ambako
alikuta ng’ombe mmoja anatoa lita 27 kwa siku na kwamba linatoa mchango
mkubwa katika uchumi.
“Nikajiuliza,
sisi Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na ng’ombe wengi Afrika, lakini
wanasaidia vipi katika uchumi wetu wakati hata viatu tunaagiza kutoka
China wakati tuna ngozi ya kutosha?” alisema.
Mauaji ya Afrika Kusini
Dk
Slaa pia amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe kuacha kufanya siasa wakati maisha ya Watanzania wanaoishi
Afrika Kusini, yako hatarini.
“Watanzania
hao wanatakiwa kurudishwa nchini haraka hadi hali ya usalama
itakaporejea Afrika Kusini. Serikali isikwepe jukumu la kuwarudisha
wananchi wake,” alisema.
Alisema anashangazwa na kauli ya Membe kwamba Mtanzania aliyekufa Afrika Kusini aliuawa kwa ujambazi.
“Unadhani
watasema ameuawa kwa sababu gani wakati hata polisi wa Afrika Kusini
wako upande wa vijana hao wanaofanya vurugu? Alitakiwa kufanya uchunguzi
wa kina ili kujiridhisha kwamba Mtanzania huyo aliuawa kwa ujambazi,” alisema.
Juzi,
Membe alikaririwa akisema kuna Watanzania watatu ambao wamekufa lakini
akakanusha kuwa waliuawa kwenye vurugu zinazoendelea Afrika Kusini.
Miongoni mwa waliokufa ni Rashid Jumanne ambaye aliuawa kilomita 90
kutoka mji wa Durban.
ACT- Wazalendo
Akizungumzia ujio wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), alisema kwa kifupi: “Nakiona
kama vyama vingine lakini siyo tishio kwa Chadema kwani chama chetu
kina misingi imara ambayo inakifanya kila siku kuwa juu,” alisema kwa kifupi
Credit: Mwananchi.
Credit: Mwananchi.
0 Comments