Kundi la Watanzania 25
limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini jana tarehe 25 Aprili, 2015
kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza
kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.
Watanzania hao walikuwa
wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini
Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha
wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Afrika Kusini.
Wakati huo huo, Ubalozi
wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania
wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini
Johannesburg.
Ubalozi umetuma Afisa
kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa
madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
25 Aprili 2015
0 Comments