Kiongozi mkuu wa
ACT-Wazalendo Zitto Kabwa anashangazwa na viongozi wa CHADEMA kuhoji
anakotoa fedha za kugharamia mikutano na ziara za ACT-Wazalendo pamoja
na kujinadi kwa wananchi.
Zitto amewajibu jibu
jepesi kwa kusema “CHADEMA walianza bila ruzuku, waulizeni fedha za
ziara zao za kuzunguka kwa helkopta nchi nzima walizitoa wapi? Kule
walikopita ndiko na mimi ninakopita huku na huko” alisema huku
akishangiliwa na maelfu ya wananchi jijini Mwanza katika viwanja vya
Furahisha
Alifafanua kuwa fedha za
chama chake wanazofanyia ziara zinatokana na michango mbalimbali ya
watu wenye nia njema na chama hicho, Zitto pia aliwataka wananchi wa
Mwanza kuchuja na kuchagua uzalendo. “Chujeni mtu mwenye hoja twendeni
tukaijenge nchi”.
0 Comments