Jeshi
la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Jumanne Yusuph (33), Mkazi wa
Kijiji cha Mtamaa ‘A’ Manispaa ya Singida kwa kumuua mama yake mzazi,
Tausi Abdalah (56) kwa kumchinja na kisu shingoni, juzi alfajiri katika
kijiji hicho.
Baada
ya kumchinja mama yake, kijana huyu alikwenda kwa mama yake mkubwa
kutoa tarifa, kisha tena akaenda kwa mwenyekiti wa kijiji kumjulisha
kuwa amefanya mauaji ya mama yake.
Kabla ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo aliwaua ng’ombe watatu wa mama yake kwa kuwacharanga na mapanga.
Pia
inadaiwa kuwa aprili 16 mwaka huu, mtuhumiwa huyo alifika kwa mama yake
na kubomoa sehemu ya nyumba yake kisha akatokomea kusikojulikana.
0 Comments