May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. Bado miezi michache ufanyike Uchaguzi Mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati
ya Jiji la Arusha umeshuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao
walikuja kwa ajili ya kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia rasmi kabisa
kwamba atagombea Urais mwaka huu.
“Watanzania
wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo..
Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya
CCM watayatafuta nje ya CCM. Sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM
tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”>>> Edward Lowassa.
“Nchi
yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu
usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. Aweze
kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walio nacho na wasio
nacho“>>> Edward Lowassa.
“Nina
hamu, nina shauku na nina uwezo wa kuiongoza Tanzania… Ninaamini nina
kila kigezo cha kuibeba dhamana ya nchi yetu.. Katika vitu
ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita ya Kagera, nilishiriki
kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele kuikomboa nchi yetu,
muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?”
“Kwa
wingi wa rasilimali tulizonazo tuna kila sababu ya kuwa ombaomba… Haya
ninayoyaeleza ndio msingi wa utendaji wa Serikali nitakayoiongoza
nikichaguliwa.. nimeamua kugombea Urais ili kupambana na umaskini..
Uongozi wangu utaleta mchakamchaka wa maendeleo”– Edward Lowassa.
“Najua
Watanzania wangapi wanaishi kwa bodaboda, mama ntilie.. hawa ni rafiki
zangu hawatafukuzwa barabarani.. ni raia wa Tanzania wanaostahili kula
kama wewe“
“Kwenye michezo tumechoka kuwa kichwa cha mwendawazimu, tutaibadili hali hii kwa kasi sana“>>> Edward Lowassa.
0 Comments