Brighton masalu
KABLA
hajaanza ‘kuuza sura’ kwenye runinga, Blandina William Wilbert Chagula
‘Johari’ alikuwa akijihusisha na kazi ya upishi na uuzaji wa chakula
biashara ambayo aliifanya jijini Dar kabla hajajiunga na Kundi la Sanaa
la Kaole baada ya kuhitimu mafunzo ya Hotel Management.
Johari alianza kupika na kuuza chakula kwenye catering ya shangazi
yake huku akihangaika kutafuta njia ya kutimiza ndoto yake ya uigizaji
aliyokuwa nayo tangu akiwa kijijini kwao Bugoyi mkoani Shinyanga.Johari
anasema aliamua kusomea masomo ya upishi kwa kushinikizwa na ndugu zake
walioamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kupika chakula kizuri na kitamu japo
moyoni mwake hakuwa na ‘hobi’ hiyo.
“Kabla ya kutimiza ndoto yangu hii ya uigizaji, nilikuwa napika na
kuuza chakula, si unajua katika maisha kabla hujatimiza ndoto na malengo
yako ni lazima uhangaike kwa kupitia vikwazo na vizingiti vingi?
“Hivyo mimi nilijikuta nikiangukia kwenye u-hotelia japo sikuwa
interested kabisa, lakini kwa sasa namshukuru Mungu kwa kuwa nimetimiza
ndoto yangu,” alisema Johari katika mahojiano maalum na mwandishi wetu
hivi karibuni.
0 Comments