TETEMEKO la ardhi
limetokea nchini Nepal na kupoteza maisha ya watu ya 900 na kuangusha
Mnara wa Karne ya 19 Mjini, Kathmandu pamoja na kusababisha maporomoko
ya theluji kutoka katika milima.
Taarifa zinadai kuna
uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo lililotokea
jana lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara
mji wa pili kwa ukubwa nchini Nepal.
Tetetemeko hilo la ardhi
ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 81
na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani kaskazini mwa
India na Bangladesh.
Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.
Naibu balozi wa Nepal
mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa mamia ya watu
wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa kila sehemu kubwa
na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali ni nchi nzima
imeathirika.
Nepal ilikumbwa na
tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo mwaka 1934
likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha yao.
Baadhi ya Waokoaji
wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo aliekuwa amefukiwa
kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma kutokana na tetemeoko
hilo.
Sehemu ya athari za tetemeko hilo.
Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.
Wananchi wa Nepal wakishirikiana kwa pamoja kuvuta kamba.
Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.
Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa Daily Mail
0 Comments