Advertisement

Responsive Advertisement

WAZAZI WAMEMLAZIMISHA MTOTO WAO AFANYE "HOMEWORK",AKASIRIKA NA KUAMUA KUWAUA KWA KISU!!

home
Matukio ya watoto kuwaua wazazi wao bado yameendelea kutoka katika maeneo mbalimbali duniani.

Sababu kubwa huenda inasababishwa na malezi ambayo hupewa na wazazi wao hadi kupelekea kuwa na tabia aidha ya kuwatishia maisha na wengine hufikia hatua ya kuwaua wazazi wao kwa sababu mbalimbali.
Stori ya leo inatokea huko Japan ambapo mtoto wa miaka 15 amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kumuua mama yake mzazi pamoja  na bibi yake ambao walimtaka kufanya kazi za shule ‘homework’ kabla ya kwenda kulala.
Mtoto huyo baada ya kufanya tukio hilo alijipeleka mwenyewe kituo cha polisi na baada ya kufanyiwa uchunguzi alikutwa na kisu chenye damu ndani ya begi lake na polisi walipofika nyumbani walikuta miili ya watu hao wakiwa tayari wamefariki.
Alipohojiwa mtoto huyo alisema aliamua kufanya hivyo baada ya kukerwa na shinikizo la wazazi wake hao kumtaka kufanya homework.
SIRI ZA MAFISADI ZIKO HAPA

Post a Comment

0 Comments