Hii
ni May 16 2015 ambapo kwa mujibu wa Wajenzi wa barabara, mmiliki wa
nyumba hii anaendelea kuishi hapa japokuwa barabara imeshakamilika.
Hii ipo hata Tanzania unakuta barabara
inabidi ipanuliwe so kuna watu tu watabomolewa nyumba zao ambazo ziko
ndani ya eneo ambako ujenzi inabidi ufanyike.
Kwenye hizi picha za leo ni kutoka China
ambako wamiliki wake wamekataa pesa zilizotolewa na idara ya ujenzi wa
barabara kama fidia,
Picha ya April 2010 huko Guangxi Province
Hii
nyumba wamiliki wake ni wazee Luo (67) na mke wake mwenye miaka 65
ambao waliingia kwenye mvutano na serikali kwa miaka minne kuhusu malipo
yao na kuhama hapa.
Hata
hivyo Luo alikubaliana na serikali na akalipwa zaidi ya MILIONI 80 za
Kitanzania ndio akakubali kuhama na nyumba ikabomolewa December 2012.
Hata
hivyo wakazi wengine waliogomea nyumba zao zibomolewe baadae baadhi yao
waliripotiwa kulipwa kiasi kikubwa cha pesa na kukubali kuondoka
kupisha ujenzi.
0 Comments