Elizabeth
Sombe anayedaiwa kunusurika kubakwa. Akizungumza na Amani juzi,
Elizabeth alisema aliamua kuja Dar kufanya kazi baada ya kukatisha
masomo yake akiwa darasa la sita kutokana na ugonjwa wa kifafa na hali
duni waliyonayo nyumbani kwao.“Siku moja nyumbani alikuja rafiki yangu
na kumwambia mama yangu kuwa amenitafutia kazi Dar hivyo nijiandae
kuondoka naye. Nilijiandaa, nikaja Dar.
KHAA!
Binti aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Sombe (13), mkazi wa
Mafinga mkoani Iringa ambaye alikuja jijini Dar kwa ajili ya kufanya
kazi za ndani, amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wodi
ya Mwaisela namba mbili, Dar baada ya kucharangwa mapanga na kundi la
vijana kufuatia kukataa kubakwa.
“Nilipokelewa na rafiki wa yule mama
Neema ambaye anaishi huku, akanipeleka kwa mtoto wake anaitwa mama
Junior. Ni Mbagala Rangi Tatu lakini naye anaishi maeneo
hayohayo.“Nilianza kufanya kazi ikiwemo kumlea mtoto, kufua, kufanya
usafi wa ndani na kupika lakini siku nyingine chakula cha mchana alikuwa
akimtuma mtu atuletee nyumbani,” alisema Elizabeth.
Jeraha
alilolipata baada ya kujeruhiwa na panga. “Siku ya tukio, ilikuwa
Jumatatu ya wiki iliyopita usiku nakumbuka, bosi wangu alinituma dukani
kununua vocha usiku kama saa tatu hivi ndiyo nikavamiwa na vijana wanne,
wakanifunga kitambaa usoni na kuanza kunivua nguo, nilijitahidi sana
kupiga mayowe kuomba msaada kwa watu wa jirani na wao walipoona napiga
mayowe wakaanza kunicharanga mapanga mpaka nikapoteza fahamu. Nilipokuja
kuzinduka nilijikuta niko hapa hospitali asubuhi, sikujua nilifikaje,”
alisema Elizabeth.
Aliendelea: “Sina msaada wowote ule kwani
hata kurudi Mbagala naogopa na sitaki kumuona yule mama machoni mwangu
maana sijamuona, naomba wasamaria wema wanisaidie kwani mpaka sasa sijui
nikitoka nitakwenda wapi kwani tangu nimekuja Dar ni miezi miwili tu
hata mshahara sijawahi kulipwa.
Jeraha
la mguuni. “Nahitaji msaada wa nauli na mavazi kwa kuwa sina nguo na
hata zile nilizokuwa nimezivaa siku ile zilikuwa zimechanika zote, bora
nirudi nyumbani nikamsaidie mama kwani nilimuacha akiwa mgonjwa na sijui
anaendeleaje maana ana ujauzito uliopilitiza miezi na alikuwa mbioni
kufanyiwa operesheni.”
Kwa yeyote aliyeguswa kumsaidia binti huyo ili aweze kurejea kwao Iringa, anaweza kutuma pesa kwa namba 0712 121330.
0 Comments