Watu wawili wamefariki
dunia mkoani Simiyu katika matukio tofauti akiwamo mtoto wa miezi mitatu
aliyenyakuliwa na fisi akiwa mgongoni mwa mama yake.
Kamanda wa Polisi wa
mkoa wa Simiyu, Gemin Mushy jana alisema kuwa mtoto Ng’wanza Samwel,
akiwa amebebwa na mama yake alinyakuliwa na fisi Mei 25, majira ya saa
1;30 jioni katika kijiji cha Ngugunu,Tarafa ya Kisesa wilayani Meatu.
Alisema katika
kufuatilia tukio hilo, mabaki ya mtoto huyo yalipatikana mita 200 tu
fisi kutoka eneo alilonyakuliwa huku kichwa, kifua, tumbo, mikono na
miguu ikiwa haipo.
Katika tukio jingine
mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la Magina Supa(20), mkazi wa
Nyaumata mtaa wa Kisiwani wilayani Bariadi, aliuawa kwa kukatwa na kitu
chenye ncha kali shingoni na bega la kushoto na mtu aliyekuwa amempakiza
kama abiria wake.
Akifafanua, Kamanda
Mushy alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 26 majira saa 1;00 jioni
katika mtaa wa Izunya, kata ya Somanda tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi
kwa mtuhumiwa wa mauaji hayo anayedaiwa kuwa abiria wa mpanda baiskeli
huyo aliyekuwa anajishughulisha na biashara ya daladala ya baiskeli.
Kamanda huyo alisema
kuwa mara baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye hajafahamika na
anasakwa baada uhalifu huo alitoroka. Chanzo cha mauaji hayo
hakijafahamika.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments