Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
SERIKALI ya Burundi
imetangaza kuwa uchaguzi wa Rais na Wabunge uliotarajiwa kufanyika mwezi
huu umeahirishwa mpaka tarehe nyingine zitakazotangazwa.
Vurugu Burundi.
Msemaji wa Rais
Nkurunziza, Wily Nyamitwe amesema kuwa tarehe hizo zitapangwa na
wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo hivi karibuni.
Mabadiliko hayo yamekuja
kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere
Nkurunziza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu.
Umoja wa Mataifa
umeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia
Burundi, hivyo kumtaka rais huyo kuachia ngazi mwezi huu kama
makubaliano ya Azimio la Arusha yalivyoelekeza.
Uchaguzi wa wabunge ulitarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (Juni 5) na wa urais ulipangwa Juni 26, mwaka huu.
CREDIT: BBC
0 Comments