MTU kwao! Licha ya kuwa staa wa muvi za Bongo, mwigizaji kiwango, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuitwa na wazazi wake kwenda kuishi nyumbani kwao, Kibaha mkoani Pwani ili kuepukana na skendo za kila mara za mjini.
Kwa mujibu wa chanzo, Wolper amewekewa msimamo huo na wazazi wake,
hususan mama yake mzazi aliyemwambia kwa kuwa ana usafiri anaweza kuishi
huko na kufika jijini Dar kwa kazi za mchana kutwa kisha kurudi Kihaba
kwa malazi na makazi.
Wolper alipotafutwa kuulizwa kuhusu hilo, alijibu: “Kweli wazazi wangu
wanapenda niwe nao karibu wakiamini nitaendelea kuwa mtoto mzuri bila
skendo, lakini inakuwa ngumu ndiyo maana utakuta mara nyingi niko kule
lakini kimakazi niko Dar, nitafikiria.”
0 Comments