Katibu wa Chama cha wachimbaji madini Mkoani Geita Golden Kainga
akizungumza jambo kwenye mkutano huo wa wadau wa Afya katika kutekeleza
azimio la nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa wa Kifua
Kikuu-TB kwenye maeneo ya migodi Unaofanyika Hotel ya GoldCrest ya
jijini Mwanza kujadili utafti uliofanyika mwaka jana katika migodi mine
katika wilaya za Kahama na Geita

Washiriki wa mkutano wa wadau wa afya wakiwa kwenye picha ya pamoja
IMEELEZWA kuwa,sababu za Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa
jamii kutopeleka huduma za afya ikiwemo kujenga kituo katika kijiji cha
Mgusu kata ya mtakuja Wilayani Geita chenye wachimbaji 9,324 wasio
rasmi wa madini mbali na kuwepo ongezeko kubwa la wagonjwa
waliogundulika kuwa na TB ni kutokana na kijiji hicho kuwa
haramu(hakijasajiliwa).
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita,Dk.Noel Makuza juzi
kwenye mkutano mkuu wa Wadau hao uliofanyika GoldCrest Hotel ya jijini
Mwanza ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azimio la nchi za Kusini mwa
Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa wa kifua kikuu kwenye maeneo ya Migodi.
Dk Makuza alisema kuwa,wameshindwa kupeleka huduma za afya kwenye kijiji
hicho kutokana na kuwa haramu(hakijasajiliwa)na kwamba watafanya hivyo
iwapo serikali itakisajili huku akidai kuwa,tayari serikali ipo kwenye
mchakato wa kukisajili ili kiweze kupata huduma stahiki zinazotolewa na
serikali ikiwemo huduma ya Afya.
''Ni kweli,kama mwezeshaji alivyosema,kwamba wakati wa utafiti wao
walifika katika kijiji cha mgusu na wakakuta hakuna huduma za afya
ambazo wakazi wa pale huzipata kwa kutembea umbali mrefu,hii inatokana
na kijiji hicho nitumie neno ni haramu maana hakijasajiliwa hivyo huwezi
kupeleka huduma kwenye kijiji ambacho ni haramu lakini kwa kuwa
serikali ipo kwenye mchakato huo kikishasajiliwa tuitapeleka huduma
hizo''alisema Dk Makuza
Dk Makuza alikuwa akichangia mada kuhusu utafiti uliowasilishwa na
Mshauri wa Afya wa Mgodi wa ACCACIA Dk.Zumbe Musiba ambaye alidai
kuwa,Watu 227 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu mwaka 2012/13
kwenye Maeneo ya Migodi ya wachimbaji wadogo katika wilaya za Kahama
mkoani Shinyanga na Geita mkoani Geita.
Kwa mjibu wa Dk Musiba,utafti uliofanyika kwenye migodi ya Kalole na
Mwaziba wilayani Kahama ulkibaini kuwa watu 54 walilipotiwa kuugua
ugonjwa wa Kifua kikuu(TB)katika maeneo hayo.
Takwimu hizo zinatokana na Utafti ulifanywa Mwishoni mwa mwaka jana kwa
kushirikisha wadau wa Afya likiwemo shirika la Kimataifa la
Uhamiaji(Internation Organization For Migration -IOM),wachimbaji wadogo
na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii..
Alisema watu hao wameripitiwa kuugua TB baada ya kufikishwa kwenye vituo
vya Afya vya kata za Lunguya na Chela kupima Afya zao kutokana na
kuishi katika migodi ambayo mazingira yake ni machafu yenye vumbi kali
na matumizi ya zebaki bila kuwa na tahadhari.
Dk.Musiba alisema asilimia 50 ya kesi za Ugonjwa wa Kifua kikuu
zilizoripotiwa katika maeneo hayo zina uhusiano mkubwa na Maambukizi ya
Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi.
"Kati ya watu tuliowahoji,Utafti unaonyesha kuwa wengi hawajui dalili za
TB hata viongozi wao hawajui dalili na chanzo cha Ugonjwa huo,Tumeona
chanzo cha ugonjwa huo ni mwingiliano mkubwa wa watu,Vumbi linalotokana
na uzalishaji wa mawe ya dhahabu,Nyumba finyu zisizopitisha hewa"alisema
Dk.Musiba.
Aidha Mratibu wa mpango wa Taifa wa Kuthibiti Kifua Kikuu na Ukoma
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Alln Tarimo amesem katika Mkutano
huo uliofanyika katika Ukumbi ya Gold Crest kwamba katika utafti
uliofanyika Katika Migodi miwili ya Nyakagwe na Mgusu wilayani Geita
unaonyesha watu 172 wameripotiwa kuugua TB.
Alisema katika Mgodi wa Nyakagwe watu 63 waligundulika kuwa na Ugonja wa
TB Mwaka 2012 na mwaka 2013 walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni watu
62.
Dk.Tarimo aliongeza kuwa katika Mgodi wa Mgusu waliogundulika kuwa na TB
mwaka 2012 ni watu 17,na idadi hiyo iliongezeka hadi kwa mwaka 2013
ambapo waliogungulika kuwa na ugonjwa huo ni watu 30.
Hata hivyo alifafanua kuwa pamoja na Nyakagwe kuwa na kituo cha Afya
hakina huduma ya Kupima ugonjwa wa Kifua Kikuu na hivyo wanannchi
hutembea umbali wa kilomita 25 kwenda kituo cha Afya Bukoli.
"Tulipofika Mgusu hapakuwa na kituo cha Afya wala huduma ya Vyoo hakuna
hatua hiyo huwalazimu wananchi wa maeneo hayo kusafiri umbali wa
kilomita 23 hadi 25 kwenda kupata tiba hiyo kwenye Hospitali ya wilaya
ya Geita na Kituo cha Afya Nyankumbu"alisema Tarimo.
Kwa upande wake Naibu meneja wa mpango wa Taifa wa Kuthibiti kifua Kikuu
Wizara ya Afya Dk.Liberate Mleoh,alisema Mpango huo unalenga kufikia
malengo ya Taifa ya kuwa na wagonjwa sifuri wa TB ifikapo mwaka 2035
kutekeleza azimio la nchi za Kusini mwa Afrika SADC la kuthibiti ugonjwa
huo kwenye maeneo ya Migodi.
Na Victor Bariety- Malunde1 blog Mwanza


0 Comments