Zaidi ya watanzania milioni kumi na moja katika milioni ishirini na tano
waliokusudiwa wamejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura kwa kutumia mfumo wa mashine za BVR licha ya changamoto
kadha wa kadha zilizo jitokeza.
Akisoma taarifa ya zoezi hilo mbele ya raisi Jakaya Kikwete, aliyeungana
na watanzania wa mkoa wa Pwani kwenye kujiandikisha, mwenyekiti wa tume
ya taifa ya uchaguzi jaji mstaafu Damiani Lubuva,amesema taayari
watanzania zaidi ya milioni kumi na moja wamejiandikisha katika mikoa
kumi na tatu huku matarajiwa yakiwa ni watanzania milioni 24
wakitarajiwa, huku mikoa kumi na moja ikiwa imesalia kukamilisha zoezi
hilo.
Raisi Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa watanzania waliojitokeza
kujiandikisha katika kijiji cha Msoga Bagamoyo mkoani Pwani, kwenye
daftari la kudumu la wapiga kura zoezi lililoanza kwenye mkoa huo, na
kuipongeza tume kwa kuendelea na zoezi hilo licha ya kugubikwa na
changamoto kadha wa kadha na kutoa wito kwa watanzania kuacha kulalamika
mara baada ya uchaguzi bila ya kujitokeza kujiandikisha na kupiga
kura.
Baadhi ya wananchi wa Msoga waliojitokeza kujiandikisha wameelezea
changamoto ya huduma ya umeme kwa aajili ya matumizi ya mashine za BVR,
ambapo wamesema watashirikiana kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa huku
mbunge wa jimbo la Chalinze mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amewaomba
wananchi kujitokeza kujandikisha na kutumia haki yao ya msingi ya
kikatiba.
Via>>ITV
0 Comments