Mbunge wa Jimbo la KIbakwe, George Simba Chawene
MATOKEO ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa wa Dodoma yametangazwa rasmi na kuwataja washindi katika majimbo hayo.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM wilaya ya Chamwino ambaye ni Mkurugenzi wa uchaguzi katika kura za maoni katika wilaya ya Chamwino yenye majimbo mawili Janeth Mashele amesema matokeo hayo hayamfanyi mshindi katika kura za maoni kujiakikishia ushindi huo kwani bado kuna vikao vya uteuzi ndani ya CCM.
Akitangaza
makoteo katika jimbo la Chillonwa,alimtaja Makanyaga Mwaka kuwa mshindi
katika kura za maoni kwa kupata kura 6,999,ambapo mpinzani wake Deo
Ndejembi ambaye alipata kura 5,500 na Mapana Elisha ambaye alipata kura
4278.
Katika
jimbo la Mtera mbunge ambaye alikuwa akitetea nafasi yake Livingstone
Lusinde aliibuka kidedea kwa kupata kura 20,724,akifuatiwa na Samuel
Malecella ambaye alipata kura 3,835 na kufuatiwa na Ulaya Stevan alipata
kura 2,731.
Wakati
huo aliyekuwa katibu wa Chadema Wilaya ya Chamwimo Lameck Lobote ambaye
alihamia CCM na kugombea ubunge ameshindwa kwa mbali kwa kupata kura
406.
Akitangaza
majimbo mwingine Katibu wa CCM mkoa Albert Mgumba ambaye ni mkurugenzi
wa uchaguzi CCM mkoa alimtaja mbunge wa Kongwa ambaye alikuwa akitetea
nafasi yake Job Ndugai kwa kuibuka kidedea kwa kura 22,599, akifuatiwa
na John Pallango kura 2,566 huku Dk. John Chilongani akiambulia kura
2,563.
Katika
jimbo la kibakwe Mbunge anayetetea nafasi yake George Simba Chawene
ameibuka kidedea kwa kupata kura 18,158 akifuatiwa na Mwanyinge Mwikola
kura 6,901 huku Akley Galawika kura 5,562.
Kwa
upande wa kondoa Mjini, Sanda Edwini kura, 2,626 ambapo aliyekuwa
akitetea kiti chake Mahita Zabein kura 1,539 na Nyangani Ahammed kura
639.
Kwa upande wa Kondoa Vijini,Dk Ashatu Kijaji ameibuka kwa kura 9,162, Lubuva Hasani kura 9,113 na Monica Mohamed kura 4,641.
Jimbo la Chemba Juma Nkamia kura 17,406,Costantino Degera kura 1,777 na Khamis Mkotya kura 1,420.
Wakati huo huo majimbo mawili majimbo mawili ya Dodoma mjini na Bahi majibu yanasuasua kutangazwa.
Katika
jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka ameibuka Kidedea kwa kupata
kura 6972 huku mpinzani wake Dk.Pius Chaya akiwa na kura 6270.

0 Comments