Tume ya Uchaguzi (NEC),
imesema imeandikisha zaidi ya watu milioni 21 nchini tangu uandikishaji
uanze Februari 23, mwaka huu na kwamba, Dar es Salaam pekee,
wameandikishwa watu zaidi ya milioni mbili.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema
juzi Dar es Salaam kuwa, uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la
Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) unaendelea jijini humo hadi Agosti 8.
Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, baada ya siku hizo zilizoongezwa, hakutakuwa na muda mwingine utakaoongezwa.
“Tumieni
muda ulioongezwa kujiandikisha, vinginevyo mtaikosa haki yenu ya kupiga
kura kwa sababu ya kutoandikishwa katika Daftari la Wapigakura,” Jaji Lubuva alisema.

0 Comments