Mgomo mwingine wa madereva nchini Tanzania unanukia kufuatia Chama cha wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU pamoja na wizara ya kazi kushindwa kutekeleza makubaliano yayolifikiwa na tume iliyoundwa na waziri mkuu kutatua mgogoro huo.
Kwa
mujibu wa naibu katibu mkuu wa TADWU, Bwana Rashidi Salehe amesema
kwamba kutokana na Wizara kushindwa kutekeleza makubaliano hayo
wanatarajia kugoma tena kuanzia Agosti tisa mwaka huu.
Amesema
kuwa madereva watagoma tena kufuatia wizara ya kazi pamoja na Sumatra
kuendelea kutumia mikataba ya zamani katika kutoa leseni wakati
makubaliano ya tume iliyoundwa na waziri mkuu yalitaka mikataba mipya
ianze kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
Katika
makubaliano yao mapya, madereva wa malori yanayotoka nje ya nchi
walikuwa wanatakiwa kulipwa mishahara ya shilingi milioni moja, huku
madereva wa daladala shilingi laki tano pamoja na posho.

0 Comments