MGOGORO
wa vyama viwili vya siasa CUF na CHADEMA ambavyo vinaunda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA), katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu,
juzi ulichukua sura mpya.
Hali
hiyo inatokana na mgombea mmoja wa ubunge wa jimbo hilo kupitia CUF,
Martine Makondo na wafuasi wake, kuvamia uzinduzi wa kampeni za mgombea
ubunge wa CHADEMA, Martine Magire ambapo mgeni alikuwa Mama Regina
Lowassa (mke wa Edward Lowassa).
Mama
Lowassa alishindwa kuzindua kampeni hizo kutokana na vurugu kubwa
zilizotokea. Awali mkutano ulikuwa ufanyike kwenye Uwanja wa Michezo
uliopo katika Sekondari ya Lagangabilili.
Dalili
za vurugu zilianza kuonekana mapema baada ya wafuasi wa CHADEMA kudai
kuwa, mgombea wa CUF alikuwa amekwenda kwenye mkutano huo na kundi la
vijana ili kuvuruga mkutano.
Baada
ya Mama Lowassa kuwasili eneo la mkutano akiwa na Naibu Katibu Mkuu
Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa (BAWACHA),Kunti Yusuph, mgombea wa
CUF aliwasili eneo hilo akiwa amebebwa na wafuasi wake wakidai mgombea
wao amehujumiwa na mgombeawa CHADEMA na kusababisha jina lake likatwe na
Kamati Kuu.
Wafuasi
wa CUF walimpandisha mgombea wao (Makondo), jukwaani ndipo vikaanza
kutokea vijembe kati yao na wafuasi wa CHADEMA wakiimba, kupiga kelele
za kuwataja wagombea wao.
Hali
hiyo iliwashangaza viongozi wa CHADEMA na mgeni rasmi (Mama Lowassa)
kwa dakika 15 ndipo walinzi wa chama hicho wakamwondoa eneo hilo
wakihofia usalama wake katika mkutano huo.
Baada
ya Mama Lowassa kuondolewa jukwaani, kupanda gari yake na kuondoka eneo
la mkutano, Yusuph alianza kuwatuliza wafuasi wa vyama hivyo bila
mafanikio akaamua kuwatuhumu wananchi, lakini wafuasi walimzomea
wakitaka Makondo arudishwe.
"Tatizo
tunafanya siasa kwa ushabiki na matokeo yake ndiyo haya, mimi sikuja
kunadi mahindi kwenye mnada, nimekuja kumwombea kura mgombea urais wa
UKAWA (Edward Lowassa), ubunge na udiwani mtajuana wenyewe Oktoba 25,
mwaka huu," alisema.
Hata
hivyo, Yusuph alishindwa kutuliza vurugu hizo na kulazimika kuondoka
eneo hilo chini ya ulinzi wa vijana wa CHADEMA na kuwaacha viongozi wa
mkoa, wilaya waendelee na mkutano lakini hata baada ya kuondoka, mkutano
huo haukuendelea.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Gemin Mushy, alisema askari wake walitumia
busara kutomtoa mgombea wa CUF kutokana na mazingira kutokuruhusu
kumkamata.
Chanzo
cha mgogoro huo ni Makondo ambaye awali alikuwa CHADEMA, kutimkia CUF
baada ya jina lake kukatwa ingawa alishinda kwenye kura za maoni na
aliyeshinda nafasi ya pili Magire kupewa nafasi hiyo.
Mpekuzi blog
0 Comments