Mrembo wa filamu za kibongo nchini ambaye ameshapitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa viti maalumu, Irene Uwoya anawashangaa wasanii wenzake ambao hawakiungi mkono chama hicho wakati baadhi yao walikuwa karibu sana na Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Uwoya amewachana
wasanii ambao wamekuwa wakisema hawaoni sababu ya kumuunga mkono wakati
yeye hakuwahi kuwathamini hata siku moja.
“Sasa narudi kwa wasaniii wasio jitambua! katika tasnia yetu, ukweli
usiopingika Kikwete amekuwa karibu sana na wasanii na ametufanya
tuthaminike.
“Lakini chaajabu kunawatu wanajifanya hawajui mchango wake, kiukweli inaumiza sana!
"Kuna watu walikuwa wanashinda Ikulu , anawasaidia sana katika kazi
zao lakini leo wamesahau yote na kumsapoti mtu ambaye hajawahi hata
kuwatambua kwanafasi zao, kama sio ushabiki maandaz niniii? Loooo!!!
aibu”.Uwoya ameandika.
Mpekuzi blog
0 Comments