Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM na mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema CCM haijakamilika kwa asilima 100 na kwamba kuna mambo machache ambayo hayako sawa lakini wanayafanyia kazi.
Nape
amesema bianafsi anaupenda sana upinzani wa vyama vya siasa hapa nchini
kwa kuwa wamekuwa wakiishtua Serikali ya CCM kwenye mambo machache
ambayo yamekuwa yakilala ama kwenda kinyume na utaratibu.
Nape
aliyasema hayo jana wakati akizindua Kampeni ya “Nimeshtuka” ambayo
inawahusisha wasanii mbalimbali ambao awali walikuwa wanachama wa
Chadema na kumuunga mkono mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowasa ambapo
kwa sasa wasanii hao wamehamia CCM.
Katika
mkutano huo, Nape alibeza uamuzi wa Lowassa kuhamia Ukawa na kuongeza
kuwa CCM imejipanga kushinda uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu.
Alienda
mbali zaidi na kuwaomba wananchi kumuombea dua Lowassa aweze kuwa na
afya njema ili Oktoba 25 aweze kushuhudia ushindi wanaoupata CCM.
Kwa
upande wake kiongozi wa wasanii hao ambao wamejitoa Ukawa, Vincent
Kigosi maarufu kwa jina la Ray alisema kuwa walipokwenda Ukawa walidhani
wanakwenda kwenye safari ya matumaini hata hivyo baadaye waligundua
safari hiyo haikuwa ya matumaini.
“Nimezunguka
na Lowassa baadhi ya maeneo lakini sijaona sera za maana na zenye
mashiko, nawaambia vijana wenzangu mimi nimeshtuka na nyie hebu
shtukeni” amesema Kigosi.
Naye
msanii wa filamu, Aunt Ezekiel aLIwataka vijana kujituma kwa kufanya
kazi kwani hakuna mtu anayeweza kuwapa mabadiliko ya maendeleo isipokuwa
ni vijana wenyewe.
ALIwashauri
vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuichagua CCM badala ya
kufuata mkumbo kwa kuamini ahadi zisizotekelezeka.
Wasanii wengine waliokuwemo kwenye Kampeni hiyo ni pamoja na Juma Nature, Inspekta Haroun ‘babu’, Kitale na wengine.
Mpekuzi blog
0 Comments