Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa ufafanuzi kuhusu tatizo la kukatika kwa umeme linaloendelea nchini linatokana na kuongeza taratibu megawati hadi zifikie megawati 335.
Meneja
Mahusiano Adrian Severin alipokuwa kwenye uzinduzi wa usambazaji wa
waya za umeme kwenye shule ya Msingi ya Msasani B,amesema tatizo la
kukatika kwa umeme litaisha Oktoba mwaka huu baada ya bomba la gesi
kujaa baa 52.
Severin
amesema Septemba 19 mwa huu Tanesco iliwasha mitambo ya Umeme wa gesi
asilia megawati 90 huku wakiendelea kuongeza kidogokidogo kufikia 335
ambazo zinatakiwa kutokana na ukubwa wa bomba hilo.
“Tatizo
hili la kukatika kwa umeme litakuwa kwenye mikoa ambayo Gridi ya taifa
imepita hivyo tulianza kuzalisha megawati 90 na tunaendelea kupandisha
kiwango taratibu ili kufikia megawati 335 mwishoni mwa Oktoba mwaka
huu,”amesema Severn.
Amesema
Tanesco wanaendelea kuongeza kupandisha kiwango taratibu za megawati
ili tatizo la kukatika kwa umeme lipungue kwenye mikoa mbalimbali
nchini.
Wakati
huohuo Shirika hilo limesambaza nyaya za umeme zenye thamani ya Sh10
milioni kwenye vyumba 18 vya shule ya Msingi Msasani B.
Severin
amesema Tanesco linajihusisha na jamii kwa kusaidia kutoa misaada
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo huduma za afya na kugawa madawati katika
shule mbalimbali.
Aidha,
Afisa Takwimu Geogre Maiga amesema msaada huo wa umeme utaisaidia shule
hiyo kusoma kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa kutumia komputa.
“Kama
umeme umeingia kwenye shule hii ninaamini kuwa ndio mwanzo wa kupata
komputa ambapo wanafunzi wetu wataweza kujifunza somo la Tehama kwa
vitendo,”amesema Maiga.
Mpekuzi blog
0 Comments