September 20 2015 nakuwa miongoni mwa Watanzania walioziona taarifa kupitia Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii kwamba Umoja wa makampuni ya mawasiliano Tanzania umetoa tamko la kupokea maagizo kutoka tume ya taifa ya uchaguzi kwamba kuanzia October 24 2015 mpaka October 26 kampuni hizi ziondoe mfumo wa DATA kwa Wateja wake wote ili kuzuia usambazwaji wa taarifa za kupotosha kuhusu uchaguzi mkuu.
Dakika chache baadae nikakutana na maneno ya January Makamba ambaye ni Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambapo kupitia Twitter page yake ambayo ni Verified aliandika >>> ‘Taarifa inayoenezwa mitandaoni kwamba mifumo ya data itazimwa tarehe 24-26 Oktoba si ya kweli. Jitihada za kuhamisha mijadala hazitafanikiwa‘
Kwenye sentensi ya pili akaandika >>> ‘Taarifa hiyo ina tarehe 19.09.2014. Waliotengeneza hawakuwa waangalifu. Pia Bw. Rene Meza, aliyesemekana kaiandika ameandoka nchini kitambo‘
Taarifa inayoenezwa mitandaoni kwamba mifumo ya data itazimwa tarehe 24-26 Oktoba si ya kweli. Jitihada za kuhamisha mijadala hazitafanikiwa
Taarifa hiyo ina tarehe 19.09.2014. Waliotengeneza hawakuwa waangalifu. Pia Bw. Rene Meza, aliyesemekana kaiandika ameandoka nchini kitambo.
0 Comments