Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa anatarajiwa kurusha makombora yake ya mwisho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu dhidi mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anayeungwa mkono na Ukawa.
Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa Dk. Slaa ambaye ameonekana kuwa nchini wiki iliyopita baada ya kukaa ughaibuni kwa muda tangu alipomvaa Lowassa na Chadema, atapanda katika jukwaa la ACT-Wazalendo kwa lengo la kuyasema yake ya moyoni.
Watu wa karibu na Dr. Slaa wamelieleza gazeti moja kubwa nchini kuwa mwanasiasa huyo mkongwe amekubaliana na viongozi wa ACT-Wazalendo na atapanda kwa mara ya kwanza katika jukwaa la kampeni la chama hicho jumatano ( tarehe 7) kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho katika jimbo la Iringa Mjini,Chiku Abwao.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa,Dr. Slaa ataendelea kuzunguka katika majukwaa ya kampeni za chama hicho huku akitarajiwa kuilipua Chadema na UKAWA kwa ujumla kwa tuhuma zinazodaiwa kuwa ni kupokea pesa kutoka kwa baadhi ya makada wa CCM ili kuwakubalia kujiunga na chama hicho.
Aidha,Dr Slaa atajiunga na Zitto Kabwe ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wake wakati wakiwa Chadema na kutofautiana na hivyo Chama hicho kumfukuza uanachama chini ya uratibu wa Dr Slaa mwenyewe.
Dr Slaa alitangaza kujiuvua uanachama wake Chadema na kustaafu siasa baada ya chama hicho kumpokea na kumpitisha kuwa mgombea urais, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Baada ya kustaafu siasa,Dr Slaa alitoweka hadharani tangu July 28 mwaka huu hadi alipoibuka mwanzoni mwa Septemba katika Hoteli ya Serena,Dar es Salaam alipofanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kujiuzulu.
Baada ya mkutano huo ambao hata hivyo uliibua maswali mengi,Dr Slaa alisafiri na familia yake kwenda nchini Marekani hadi hivi karibuni aliporejea nchini
Mpekuzi blog
0 Comments