Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya
Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na
Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.
Taarifa Rasmi ya serikali kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata
Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika
Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa
matibabu.
Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015
na tangu kipindi hicho amendeleza kupata matibabu katika hospitali Hiyo
ya Apollo.
Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari nu Mitandao ya kijamii
kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.
Imetolewa na Assah Mwambene,
Msemaji Mkuu wa serikali
0 Comments