Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.
Miaka 52 imetimia tangu Tanganyika (sasa Tanzania), kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza, Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya yamefanyika uwanja wa uhuru hapa Dar es salaam,Rais
Jakaya Kikwete amekagua gwaride la vikosi mbalimbali vya ulinzi na
usalama ambavyo pia vimetoa heshima kwa kiongozi huyo kwa mwendo wa pole
na haraka.
kikosi cha anga pia kimetoa heshima zake na burudani
mbalimbali ikiwamo ngoma na michezo ya halaiki. Sherehe hizi
zimehudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wa ndani na nje ya nchi,
wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika maadhimisho haya kwa mwaka jana, yaliyohudhuriwa na viongozi
14 wa kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),
Rais Kikwete aliwataka Watanzania kujivunia na kuyaenzi mafanikio ya
kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyopatika tangu nchi ilipopata uhuru.
0 Comments