Melody za wimbo huo
ambao kwa Tanzania unaitwa ‘Mungu Ibariki Afrika, zimetoka kwenye wimbo
uitwao “Nkosi Sikelel’ iAfrika”, neno la lugha ya Xhosa lenye maana
hiyo hiyo pia).
Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu kwenye shule ya misheni ya jijini Johannesburg.
Enoch Sontonga |
Wimbo huo ulianza
kutumika kama wimbo maalum wa hekaheka za ukombozi wa Afrika na baadaye
kuanza kutumiwa kama nyimbo za taifa za nchi tano barani Afrika,
zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baada ya kupata uhuru.
Zimbabwe na Namibia
zimepata nyimbo zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa unatumika
Tanzania, Zambia na tangu mwaka 1994 kama sehemu ya wimbo wa taifa wa
Afrika Kusini.
Hata hivyo
ikumbukwe kuwa Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuutumia
wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961 pale ilipokuwa Tanganyika na
kuendelea nao baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964
Tafsiri ya mashairi ya awali yaliyokuwa kwa lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na kundi la watu.
Wimbo unaotumiwa na
Afrika Kusini hata hivyo ni mchanganyiko wa “Nkosi Sikelel’ iAfrika” na
“The Call of South Africa” (unaojulikana kwa lugha ya Afrikaan kama
“Die Stem van Suid Afrika”).
20 April, 1994
ndipo ilipotangazwa kwamba zote Nkosi Sikelel’ iAfrika na Die Stem ziwe
nyimbo za taifa za Afrika Kusini. Wimbo uliounganishwa ulianza kufanya
kazi October, 1997, baada ya maneno ya Kiingereza yalipoongezwa na wimbo
kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
0 Comments