Miili 14 ya
waliopoteza maisha katika ajali hiyoiliyotokea jana imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini .
|
Watu 13 aiwemo askari wa
kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha jana baada ya kugongwa na basi la
kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka mkoani Kigoma kwenda Dar es Salaam katika
kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku wa jana April 28,2014.
Ajali hiyo ilitokea baada ya
ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza
maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali
huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry
na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza
maisha eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea
mkoani Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva
wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha
katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja
na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.
0 Comments