Chama cha Wananchi
(CUF) kimesema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea
na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), wanastahili kujiuzulu au
kufukuzwa ndani ya vyama vyao.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mnadhimu wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin kusema kuwa
Wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza
hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na
Serikali ya Umoja wa Kitaifa au vinginevyo.
Salmin aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja kwa kuwa
wanaona kwamba lengo la kuundwa kwake halina dalili njema kwa siku za
usoni.
Jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na
Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Abdallah Bimani alisema: “Kimsingi
mpango huo unakwenda kinyume na uamuzi wa vyama vya CCM na CUF ambao
ulipitishwa na kuridhiwa na vikao vya juu vya vyama hivyo viongozi
wanaopinga jambo hilo wanaonyesha kupingana na uamuzi wa vyama vyao.”
Ajenda ya siri
Mkurugenzi huyo wa CUF alikana chama chake kuwa na
ajenda ya siri ya kuvunja Muungano au kuyasambaratisha Mapinduzi ya
Zanzibar na kusema kinachopiganiwa ni muungano wenye usawa, haki na
heshima kila upande wa washirika.
Kuhusu Ukawa kususia Bunge Maalumu la Katiba,
Bimani alisema chama chake kimetoa masharti matatu yanayopaswa
kuzingatiwa kabla ya kubadilisha msimamo wake.
Alitaja masharti hayo kuwa ni kuijadili Rasimu ya Katiba kama iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba; wajumbe wa CCM kuacha matusi, vijembe na ubaguzi na hilo lithibitishwe kwa maandishi na viongozi wake wa kitaifa.
Alitaja masharti hayo kuwa ni kuijadili Rasimu ya Katiba kama iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba; wajumbe wa CCM kuacha matusi, vijembe na ubaguzi na hilo lithibitishwe kwa maandishi na viongozi wake wa kitaifa.
Jambo la tatu ni kuhakikishiwa kuwa vikao vya
Bunge vitumike kujadili rasimu na si sera za vyama vya siasa kwa vile
ndiyo mwanzo wa kukaribisha malumbano na kusababisha Bunge kupoteza
mwelekeo na kuweka nyufa katika Umoja wa Kitaifa.
Mbatia alaani
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amelaani kauli zilizotolewa na viongozi wa CCM katika mikutano yake ya Unguja na Pemba.
Mbatia alisema kuwa hoja ya CCM kutaka kufuta
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inapaswa kulaaniwa kwani italeta
machafuko. “Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM na CUF tu, ni ya
wananchi wote, ni makosa makubwa kudhani kuwa Serikali hiyo ni ya vyama
hivyo viwili. Ilifanyika hivyo ili kutokuendelea umwagaji damu,” alisema
Mbatia.
Mbatia alisema madai ya CCM kuwa Maalim Seif
hatalipwa mafao yake hayana msingi wowote kwa sababu anacholipwa ni haki
yake. “Kwani hayo mafao ni ya CCM au wanaolipa kodi ni CCM tu? Ukweli
ni chanzo cha amani na haki ni msingi wa amani, ukweli utatuweka huru.”
0 Comments