Dk. Hamis Kigwangala,
MBUNGE
wa Nzega mkoani Tabora, Dk. Hamis Kigwangala, amesema anatafakari kama
ataweza kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu
zilizoenea kwenye baadhi ya mitandao ya jamii na kuibua mijadala
inayomshawishi kugombea urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala alisema
anatafakari jambo hilo zito na muda utakapofika atazingatia maoni ya
wananchi.
Alisema haoni hatari kwake kutangaza mapema kwamba atagombea urais ni
kujipunguzia sifa ndani ya chama chake, huku akisisitiza kwamba
hajatangaza kama anataka urais wala hajamtuma mtu kumfanyia kampeni.
“Watanzania wanaongozwa na katiba yenye uhuru wa kujieleza na kutoa
maoni, na hayo ni mawazo yao… wanayo haki ya kufanya hivyo, siwezi
kuwapinga,” alisema Dk. Kigwangala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge inayoshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Hivi karibuni uliibuka mjadala kwenye mitandao ya kijamii na baadhi
ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala
achukue fomu ya kugombea urais ifikapo mwaka 2015.
Mjadala huo ulianzishwa kwenye mtandao na kupewa jina la ‘Citizens
for Kigwangala’ ambapo wanammwagia sifa mbunge huyo kwamba ndie kiongozi
anayefaa kuwakilisha CCM katika uchaguzi mkuu.
0 Comments