Na Issa Mnally
UNGEBAHATIKA kumuona mwanaume mmoja, mkazi wa Sharif Shamba, Ilala jijini Dar, Beda Mloka ‘Baba Tony’ alivyokuwa ametapakaa damu chapachapa, lazima uulize kulikoni ambapo jibu ni moja tu la kushangaza, kisa cha yote hayo ni fumanizi, Risasi Mchanganyiko lina kisa cha kusikitisha.
Habari kamili zilizonaswa na gazeti hili ni kwamba mwanaume aliyetajwa kwa jina la Baba Asha alidai kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba Tony akiwa gesti na mkewe (jina linahifadhiwa), tayari kwa ‘kugagadua’ naye amri ya sita. Tukio hilo la aibu ya milenia lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya Pumzika iliyopo maeneo ya Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada ya kumtia mikononi ‘mwizi’ wake ambaye mbali na urafiki pia ni majirani, ndipo akamchakaza sura vibaya na kumsababishia kuvuja damu chapachapa.
NI MCHEZO
Habari za kina zilidai kuwa mke wa Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara ukaingia ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe akachukua kilongalonga hicho na kuufungua ujumbe huo.
0 Comments