Mahabusu wa Gereza Kuu
la Mkoa wa Arusha, jana walizua tafrani katika viwanja vya Mahakama ya
Hakimu Mkazi jijini hapa, baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye
basi wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa
kinyemela.
Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao
yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel (26) na
Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za heroini na misokoto
300 ya bangi, Aprili mwaka huu.
Mahabusu hao walikuwa wakipaza sauti kupinga
madaraja kati ya wenye nacho na wasio nacho kwa wengine kuachiwa na
wengine kubaki ndani kwa kisingizo cha ‘upelelezi haujakamilika’.
Huku wakipaza sauti zao kwa nguvu, mahabusu hao wa
kesi za mihadarati ikiwamo mirungi na bangi, wizi wa kutumia silaha na
mauaji, walisema wamekaa mahabusu kwa zaidi ya miaka miwili, lakini
hawajawahi hata kusomewa maelezo ya awali na kuendelea kuteseka
gerezani.
Sauti ilisikika kutoka ndani ya basi: “Wenzetu
hata mwezi haujaisha wanafutiwa kesi, jamani sisi tumekosa nini?
Tunataka haki itendeke kwa wote.”
Mahabusu hao walionekana wakiwa wamesimama ndani ya basi hilo bila nguo, huku umati wa watu waliofika mahakamani hapo ukitazama.
Baada ya kuona umati wa watu unazidi kuongezeka
kuwashangaa mahabusu hao, askari wa magereza waliondoa basi hilo eneo la
Mahakama.
Kuachiwa watuhumiwa
Taarifa za kuachiwa kwa watuhumiwa hao wa dawa za
kulevya waliokuwa na kesi mbele ya Hakimu Mkazi Arusha, Mwakuga Gwanta
zilidaiwa kuwa zilitokana na Ofisi ya DPP Arusha, kubadilisha hati ya
mashtaka.
Ilidaiwa kuwa badala ya kudaiwa kuwa walikutwa
wakisafirisha dawa za kulevya, iliandikwa kuwa walikutwa na dawa hizo
mashtaka ambayo yana dhamana.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za
Kulevya, Godfrey Nzowa alisema jana kuwa ofisi yake haina taarifa za
watuhumiwa hao kupewa dhamana lakini alisema kulikuwa na jaribio hilo.
“Ninachojua kesi hii ilipangwa kutajwa Aprili 29,
mwaka huu, lakini ikasogezwa mbele hadi Mei 2 na kilichofanyika hati ya
mashtaka ilibadilishwa na kuandikwa wamepatikana na dawa za kulevya.
0 Comments