Staa wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel
Mkali wa sinema za Kibongo, Aunty Ezekiel amesema anatamani iwe
leo au kesho apate mtoto kwani umri wake unaruhusu.Akipiga stori
mbili-tatu na paparazi wetu, Aunty alisema kuwa anatamani kuwa mama si
kwa kufuata mkumbo bali anataka kuwa mama kwani sasa ni muda muafaka
kwake.
“Natamani kwelikweli na mimi
siku moja niwe mama wa mtoto sema tu sijabahatika kupata ila naendelea
kumuomba Mungu ili ndoto zangu ziweze kutimia,” alisema Aunty Ezekiel.

0 Comments