Joto la ushindani kati ya wasanii wa Tanzania linazidi kupanda huku mashabiki na vyombo vya habari wakidaiwa kuchochea kuni kwa namna moja au nyingine.
Diamond Platinumz ambaye ndiye msanii anaekabiriwa na ushindani
mkubwa zaidi kwa sasa kwa kuwa yuko mstari wa mbele zaidi wa mafanikio
katika muziki hapa nchini na kuvuka mipaka kuiwakilisha Tanzania,
amewashauri wasanii wanaotaka kushindana nae kutojikita katika ushindani
wa nyumbani.
Diamond alifunguka katika mahojiano aliyofanya na The Jump Off ya
100.5 Times Fm na Jabir Saleh kabla hajapokea tuzo ya AFRIMMA kama
mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki.
“Tutanue mawazo, tuache mawazo ya kushindana wenyewe kwa wenyewe
Tanzania. Labda kuleta mabadiliko yataleta mabadiliko ya Chalinze,
mababadiliko ya Dar es Salaam au wapi. ‘Tukakomeshana tukikutana kwenye
show labda ya Mwembe Yanga,’ tuache hizo fikra.” Alisema Diamond.
“Kwa sababu sisi tunaweza tukafikiri hapa kuna pesa nyingi sana
lakini hakuna pesa nyingi kama ukifirikia kule mbele. Kwa sababu mbele
unaweza kupiga show mpaka dola 100,000 ambayo ni kama milioni 160 au
170. And that’s the only way we can make a lot of money.
“Nafikiria huu ni wakati wetu sisi, tufocus sasa na mbele kuliko
kufocus hapa tunakuwa tunabishana sehemu ambayo ni padogo. Hapa tu
kwenye chumba kimoja tunang’ang’ania humuhumu, huyu kashika mlango
hatoki…wakati huku kuna sebule kuna nini…” Aliongeza.
Mkali huyo wa MdogoMdogo ameeleza kuwa wakati akiwa katika tuzo za
BET alikuwa anaona jinsi ambavyo baadhi ya watu walivyotengeneza makundi
na kuanza kumdiss bila sababu. Lakini yeye kwake hiyo huwa inampa nguvu
zaidi ya kuwaza kuwa ni muda wa kuwakomesha kwa kutoa vitu vikali
zaidi.
0 Comments