Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.
******
Imeelezwa
kwamba Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk
(pichani) waliokamatwa wakiwa na Watanzania wanaotuhumiwa kwa
kukutwa na madawa ya kulevya wametoroka nchini. ******
Watuhumiwa
hao walikamatwa Februari 21, 2011 wakiwa na madawa ya kulevya yenye
thamani ya shilingi bilioni 6.2, Mbezi Beach maeneo ya Jogoo
jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema
kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo inayotarajiwa
kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa kwa
watuhumiwa hao.
Kesi
hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa
kuwa Wapakistani hao walikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia na
kupambana na madawa ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila
kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Imeelezwa
kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4,
mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata
hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa
hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie
mahakamani hapo.
Watanzania
waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana
ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji
ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa
yenye namba 3406355.
Februari
21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata
Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi
Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya
kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
0 Comments