Advertisement

Responsive Advertisement

Duh Ni kweli Nay wa Mitego yuko serious na namba 966 mpaka kuichukulia gari?


Nay wa mitegoKama wewe ni msikilizaji wa nyimbo za mkali wa bongofleva Nay wa Mitego nina uhakika utakua umeisikia sana namba 966 ambayo huitaja sana kwenye mashairi yake lakini mpaka sasa hajawahi kusema ina maana gani.
Kwenye exclusive na bongo na matukio  juzi Nay alisema kuna siku tu atakuja kueleza maana ya hii namba pamoja na baadhi ya alama ambazo amekua akizitumia kwenye picha zake za video ambazo zimesababisha Mama yake mzazi kumuita na kutaka amweleze zina maana gani manake amekua akisikia watu wengi wakimwambia kuhusu mwanae.
Screen Shot 2014-09-06 at 9.46.47 PMPamoja na kwamba wengi walianza kuzihusisha hizi alama na hii namba imani ya kuabudu Miungu, Nay amesema hayuko kwenye dhehebu lolote ambalo linaabudu Miungu, watu wavute subira iko siku atasema kila kitu ikiwemo mipango yake na hii namba ambayo inaonekana ameiandalia kitu kikubwa mpaka kulichukulia gari lake jipya.
Hii namba unayoiona hapa kwenye picha ya kwanza haijamuangukia bahati mbaya bali alifanya namna mpaka akaipata wakati wa kwenda kusajili gari lake kwenye mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
Screen Shot 2014-09-06 at 9.46.55 PM