Hatimaye
Diamond Platnumz amefunguka kuhusu tetesi zinazoendelea kuwa ameachana
na Wema Sepetu na kwamba ana mpango wa kufunga ndoa na Meninah, Diamond
alisema kuwa tetesi hizo zimekuwa zikimhuzunisha kwa kiasi kikubwa.
“Unajua hizi habari kiukweli zimekuwa zikinihuzunisha sana,” amesema superstar huyo wa muziki wa Bongofleva Tanzania.
“Unajua
mie ni mtu mmoja ambaye sipendi kuzunguzia mambo ya rumors, siju
magazeti huwa sipendi kuzungumzia kabisa, kwa kuwa najua kabisa siwezi
kubishana na media kwakuwa media ni kubwa, maana najua utaongea na huyu
na yule siku ya siku utagombana na watu. Ndio maana huwa nakaa kimya,” ameongeza Diamond anayetusua shows katika nchi mbalimbali ndani na nje ya Africa kwa sasa.
“Kusema
ukweli hili suala limekuwa likiniumiza ‘eti sijui kuna vikao vya harusi
mie nataka kumuoa Meninah’. Kusema ukweli sina mahusiano na Meninah.
Kila mtu anajua mie nina mahusiano na Wema.
“Wema
ndo mpenzi wangu, ila wakati mwingine nakuwa naelewa ile inakuwa ni
trick ya kibiashara. Mtu anajua hata nikimuandika vipi ‘Diamond sijui
kafanya nini watu hawawezi kumchukia!
Kwahiyo wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kwa watu kuwa nipo na mwanamke wangu halafu namsaliti” alisema Diamond na kuongeza
“Unajua
kitendo hicho hatimaye kinaniudhi naona mtu yupo na mpenzi wake halafu
anamsaliti. Najua hicho ni kitendo ambacho kila mtu hakimpendezi.
“Kwahiyo
wanaamua kunitengenezea chuki na maadui kupitia njia hiyo. Labda wana
wasanii wao, sasa wanaona tukiingia kwa njia hii tutaweza kuamharibia
Diamond. Ndio siku zote nimekuwa kimya tu ila sina mahusiano na Meninah.
Mie nikiwa na mtu huwa sifichi naweka wazi kabisa.
Hata
kama leo nimeachana na Wema nasema tu, why nifiche? Mie katika mambo
yangu huwa simuogopi mtu kama ningekuwa nataka kuoa basi ninge weka wazi
why nifiche??”
0 Comments