UMOJA
wa Katiba ya Wananchi “Ukawa” wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, kuzuia mikutano ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Abdulrahaman Kinana, kama alivyozuia mikutano na maandamano ya vyama
vya siasa vinavyoundwa na Ukawa.
Hayo
yamezungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Lissu wakati akizungunmza na waandishi wa habari leo, makao
makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam .
Aidha
umoja huo umetoa tamko juu ya amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu
mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba kwa kumuunga mkono Saed Kubenea
aliyekuwa amefungua kesi ya kuitaka
Mahakama
Kuu itoe ufafanuzi wa mamlaka ya bunge hilo kwa mujibu wa kifungu cha
25 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, sura ya 83 ya sheria za nchi
yetu.
Baadhi ya viongozi wa Ukawa, kuanzia kushoto ni Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba na John Mnyika.
Baadhi ya viongozi wa Ukawa, kuanzia kushoto ni Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Prof. Ibrahim Lipumba na John Mnyika.
0 Comments